Sunday, February 1, 2015

DIAMOND,ZARI WAFANYA MAAJABU MIAKA 38 YA CCM SONGEA


MSANII wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, mapema leo alipata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha la kuazimisha miaka 38 ya chama cha CCM lililofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji Songea mjini, huku akiwa ameambatana na mpenzi wake Zarinah Hasssani 'Zarithebosslady', ambapo maadhimisho hayo yamefanyika mchana wa leo, yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Mrisho Kikwete, huku yakihudhuliwa na wakazi kibao wa mji huo, ambao walifurika katika Viwanja hivyo na kufurahia shoo mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wasanii kibao wa mji huo na wengine wa Dar es Salaam, waliongozwa na Diamond.

Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti akisalimiana na Zari Mpenzi wa Diamond.

Diamond Platnumz na madansa wake wakifanya vitu vyao kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati wa sherehe za miaka 38 ya CCM leo.

Diamond akiimba pamoja na mwanamuziki Abdul Misambano wa kundi la TOT katika sherehe za miaka 38 ya CCM mjini Songea leo.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea tayari kwa kufanya onesho kubwa kwenye sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zinazofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Dk. Jakaya Kikwete wamehudhuria.
 


Umati wa wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...