Monday, February 2, 2015

BONDIA FRANCIS CHEKA ATUPWA JELA MIAKA 3

Bondia Francis Cheka (aliyenyanyua mkono), akiwa kwenye gari dogo la Magereza na baadhi ya wafungwa wengine muda mfupi baada ya kusomewa hukumu yake mapema leo katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro,chini ya Hakimu wa Mahakama hiyo Said Musuya.

HATIMAYE Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa Bongo, Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya Sh. millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake (Cheka) iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro Mjini.
Akimsomea mashitaka, Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alisema Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake aitwaye Bahati Kabanda 'Masika'.
Alisema kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka jana ambapo meneja huyo alikwenda kwenye baa hiyo kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo.
Hakimu Msuya alisema kuwa Cheka alikataa kumlipa na kumshushia kipigo kilichosababisha kulazwa hospitalini.
Baada ya hukumu hiyo huku Cheka akipandishwa kwenye difenda tayari kupelekwa gerezani akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote, mashabiki wake walimvaa meneja huyo wakitaka kumshushia kipigo hivyo kuibua taharuki mahakamani hapo.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakisema wapo tayari kujichanga ili kukata rufaa wakiamini kuwa bondia huyo ameonewa.
Mbali na hukumu hiyo mahakamani hapo, kulikuwa na kesi nyingine mbili zilizokusanya umati, moja ikiwa ni ya Sheikh Ponda juu ya uchochezi na ile ya mtoto wa boksi inayowakabili baba na mama Nasra
 Cheka akipanda kwenye gari la Magereza tayari kwa kwenda kutumikia kifungu hicho.
Mmoja wa Askari waliokuwa wamemuweka chini ya ulinzi Bondia huyo akimpokonya simu yake tayari kwa kwenda Gerezani.
 Cheka akijiandaa kudandia gari la Magereza.
...akimchimbia mkwara mmoja wa mapaparazi waliokuwa wakipiga picha za tukio hilo.
Askari akichukua baadhi ya vitu alivyokuwa navyo Bondia huyo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...