Saturday, January 31, 2015

PELLEGRINI: DIEGO COSTA ANATAKIWA KUBADILIKA!


 
Faulo iliyomgharimu Costa wa Chelsea kwa kumkanyaga Can wa Liverpool wakati wa mchezo wa Capital One mapema wiki hii
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ametoa ya moyoni juu ya kufungiwa kwa straika wa Chelsea, Diego Costa kwa kumtaka abadilike ili kuendeleza kipaji chake. 

Pellegrini aliyaongeza hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England wakati timu hizo zitakapomenyana leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

 Costa, 25, atakuwa jukwaani leo pamoja na mechi dhidi ya Aston Villa na Everton akitumikia adhabu aliyopigwa na Chama cha Soka England, FA, la kukosa mechi tatu kwa kosa la kumkanyaga maksudi kiungo wa Liverpool, Emre Can wakati wa mechi nusu fainali ya Kombe la Ligi ‘Capital One’, kitendo ambacho Pellegrini amesema: “Hatakiwi kucheza katika aina ile ya uchezaji wake kwa kuwa yeye ni mchezaji mzuri sana.”

Mbali na tukio hilo, Costa amekuwa akitajwa kwa ugomvi uwanjani ambapo mara kadhaa amekuwa akikwaruzana na wachezaji timu pinzani huku mpaka sasa akiwa amezawadiwa kadi za njano nane msimu huu.

 Kuhusu mechi yao ya leo, kocha huyo raia wa Chile, alisema: "Sio mechi ya kuamua ubingwa, sababu baada tya mechi yenyewe kuna pointi 45  tunapigania pia. Na ikumbukwe kuwa tuliwahi kutwaa ubingwa  baada ya kuwa nyuma kwa pointi nane nyuma ya Manchester United, tukiwa tumebakiza mechi sita tu (ilikuwa msimu wa 2012)".

"Kwa hiyo katika soka, huwezi kujua. Lakini mechi hii ina umuhimu sana  ambayo itatufanya tupunguze gepu kati yetu na wao kileleni."
 
Moja ya matukio ya Costa katika mchezo huo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...