Friday, January 30, 2015

JACK WA MAISHA PLUS ATUNDIKWA MIMBA NA MWARABU


Msanii wa filamu ambaye ni zao la Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan.

MSANII wa filamu ambaye ni zao la Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan anadaiwa ni mjamzito huku mlengwa wa mzigo huo akidaiwa kuwa Mwarabu aliyewahi kuripotiwa kuwa anatoka naye.

Jack alitua hivi karibuni akitokea Dubai alikokuwa akiponda maisha na mara kadhaa amewahi kutundika picha mtandaoni akiwa kimahaba na mwanaume huyo wa Kiarabu.
Akizungumzia madai hayo, Jack alisema: “Mimi ni mwanamke bwana, kuzaa ni wajibu kwa hiyo sioni kama ni skendo mimi kuwa na mimba.”
Alipoulizwa kama ni ya mwanaume Mbongo au yule Mwarabu wake, mwanadada huyo alipata kigugumizi na kuishia kusema: “Msubiri nikijifungua.”


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...