Friday, April 11, 2014

JOKATE AHAMISHIA KIDOTI CHAKE KWENYE NDALA

Picha ya bidhaa mpya ya ndala ya Kidoti.

Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini, Jokate Mwegelo amefunguka kwa kusema kuwa ameamua kufungua biashara ya ndala za brand yake ya ‘Kidoti’ kutokana na mapenzi yake ya uvaaji wa ndala kataki maisha yake ya kawaida .

“Mimi napenda kuvaa ndala, napenda kuvaa wakati nakwenda kushoot,siwezi kuvaa high hills wakati nashoot, wakati unapakwa make up unaonaee, unatengenezwa nywele, you cannot wear hills lazima uwe umevaa kitu comfortable,”.

“Kwahiyo nikaona kwamba ndala ni kitu kizuri,napenda kuvaa ndala,ni kitu easy,kuvaa rahisi halafu ni kitu ambacho watu wanakihitaji why not have ndala ambazo zina mvuto wa kipekee? Kama nilivyohaidi watu kwamba Jokate kupitia brand ya Kidoti itaanzisha bidhaa mbalimbali kukidhi mahitaji ya watu na jamii mzima.


Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini, Jokate Mwegelo.

Nashukuru kuna support kwa Kidoti yenyewe kama brand. Kwahiyo tutaendelea kutoa vitu mbalimbali vya kufurahisha. Unajua kutoa surprise ni njia moja wapo ya kufurahisha, hawakutegemea kupata kitu kuzuri lakini wamekipata. Kwahiyo ni mambo ya Kidoti hayo ni bidhaa nzuri waipokee na tutaendelea kutoa bidhaa mbalimbali.” aliongeza.

Pia Kidoti amesema kuwa bidhaa ya ndala ya Kidoti itapatikana Tanzania nzima.
“Tutasambaza Dar es salaam nzima na mikoani,kwahiyo ni kitu ambacho kipo katika mipangilio ya kusambambaza sehemu mbalimbali ili upatikanaji uwe rahisi na tunafanya jitihada za kutangaza sehemu ambazo zitakuwa zinapatikana.”

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...