Friday, March 14, 2014

UKWELI KUHUSU BEEF LA ODAMA NA SHAMSA FORD HUU HAPA
Odama Jennifer Kyaka ambaye ni star mkubwa wa filamu nchini amekanusha habari kuwa yupo katika beef na star mwenzake wa filamu Shamsa Ford. Karibia mwezi sasa baadhi ya mitandao na magazeti yamekuwa yakiandika kuwa Odama na Shamsa hawaelewani kama mwanzo kisa kikidaiwa ni Shamsa kuchelewesha mchango wa harusi ya mdogo wake Odama kinyume na taratibu na alivyoarifiwa tangu mwanzo. Hata hivyo akichonga na Swahiliworldplanet Odama alisema hana tatizo kabisa na Shamsa na wanaelewana kama kawaida "ni uongo wanaosema hivyo, sina tatizo na Shamsa na ningependa watu wasizushie wenzao mambo ambayo hayapo na hayana ukweli" alisema Odama ambaye amejizolea umaarufu pasipo kuwa na skendo za hovyo kama baadhi ya mastaa wenzake walivyo.

Kwa upande mwingine filamu mpya ya Odama inayoitwa JICHO LANGU kutoka kampuni yake ya J-Film 4 Life itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu kwa hiyo kaa tayari kununua nakala yako halisi.


Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...