Monday, March 24, 2014

ROSE MUHANDO KUFANYA TAMASHA LA UPENDO

Rose Muhando ambaye anamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji anatarajia kufanya tamasha la UPENDO katika ukumbi wa wa kanisa la Baptist Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 06/04/2014, tamasha litaanza saa 7:00 mchana na kuendelea.
http://3.bp.blogspot.com/-uVpFLAt2Bmk/T4zS9Z9QIAI/AAAAAAAADFU/2p-ToGCMP3c/s1600/IMG_6572.JPG

 Lengo zima la kuandaa tamasha hili ni kukisaidia kituo cha watoto yatima cha HOCET kilichopo  Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam.  Kabla ya tamasha Rose Muhando atakwenda kukitembelea kituo hicho kwaajili wa kuwafariji na kuwatia moyo watoto hawa ambao wametoka katika mazingira magumu baada ya wazazi wao kutoweka dunia. Rose Muhando amesema atatoa msaada wake kama vile Mungu alivyomjalia. Kutakuwa na wasindikizaji watakaomuunga mkono malikia huyo wa muziki wa injili Tanzania Rose Muhando ni  waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania,  Stella Joel, Elizabeth Ngaiza na Janeth Mrema. |

Kuna nafasi ya kutosha kwako wewe ya kuweza kuungana na baraka hizi na kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Rose Muhando kwa kutoa kile ulichonacho ili watoto hawa ambao ni yatima waweze kujiona kama kuna watu wanaowajali na kuwatunza. Watoto hawa wanauhitaji wa vitu vingi kama vile mavazi, chakula, vifaa vya shule, matibabu na mengine mengi. Mungu amekujali kuwa na kidogo ulichonacho, ni vizuri ukashirikiana na hawa watoto wenye uhitaji ili Mungu aweze kufanya jambo katika maisha yako na kufungua milango iliyofungwa na adui yako kimafanikio.
Katika tamasha hili kutakuwa hakuna kiingilio, ila ni wewe kuja na sadaka au mchango wako kwaajili ya kuwasaidia hawa watoto yatima. Kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama vile Stella Joel, Elizabeth Ngaiza, Julieth Dougras, Janeth Mrema, Christopher Malango, Tuamini Njole, Sifa John, Faraja Ntaboba, Kwaya ya Baptist  Magomeni, Kwaya ya Ukombozi, Subi Mwamezi, Christina Matai, John Shabani, Ado Novemba, Gideon Mutalemwa na Petro Mwampashi. Waimbaji hawa wameamua kujitolea kwa lengo la kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele. Watamtumikia Mungu siku hiyo na watachochea IMANI yako kuzidi kukua na kumtumainia Mungu wetu.

Bwana Yesu Kristo amehimiza sana katika kitabu kitakatifu (BIBLIA) juu ya upendo. Mimi na wewe tutakiwa sasa kuonyesha upendo  wetu kwa hawa yatima ambao ni walengwa wa siku hiyo. Na uppendo huu utakaouonyesha siku hiyo ukazidi kufanyika na kwa watu wengine.

Kama umeguswa basi unaweza kuwasilisha mchango wako katika ofisi za RUMAFRICA zilizopo Sinza Afrikasana eneo la soko la mbogamboga na matunda  au wasiliana na Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Elizabeth Ngaiza kwa simu +255 0714 294076 au 
Stella Joel +255 0756 846166

WATAKAO MUUNGA MKONO ROSE MUHANDO KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOTOKA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
http://4.bp.blogspot.com/-d7R5tn4LwFE/ULD1Ig84iVI/AAAAAAAAANA/Zn3HYOhxi_Y/s1600/DSC_0134.JPG
Janet Mrema
http://3.bp.blogspot.com/-5TRvCOoRd7Q/UYFbSh6shnI/AAAAAAAAJSA/xgfRdd1T64w/s640/DSCN9611.JPG
Stella Joel
http://4.bp.blogspot.com/-5lD3n4nN4iU/UuNo9BG1nrI/AAAAAAAAVgc/X5rZZIh4Ha4/s1600/16.jpg
Elizabeth Ngaiza

KUTOA NI MOYO

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...