Afisa Uhusiano wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania Jane Matinde, (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu PhilemonNathaniel Mgaya aliyejishindia shilingi milioni tano (5m/-) ikiwa ni zawadi ya wiki katika promosheni ya Mimi ni Bingwa. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishini mwa wiki katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu ashinda kwenye promosheni ya Airtel Tanzania Mimi ni Bingwa
MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu PhilemonNathaniel Mgaya anakila sababu za kuwa na furaha baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni tano (5m/-) za Airtel Tanzania Mimi ni Bingwa promosheni zinazotolewa kila wiki.
Hili linakuja wakati bado wiki chache tu kampuni hiyo ya mawasiliano kutangaza mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 ambaye atapatikana katika kilele cha promosheni hiyo. Akizungumza wakati wa droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Jane Matinde, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania alisema matokeoi mazuri ya promosheni hiyo inadhihirisha dhamira na jitihada za kampuni za kuwasaidia wateja wake.
“Airtel kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa leo hii inaendelea kuzawadia wateja wengine, tukielekea katika droo kubwa ambayo itachezeshwa hivi karibuni, droo itakayomwezesha mshindi mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 50.
“Philemon Nathaniel Mgaya ambaye anapokea hundi yake leo hii, ni mmoja kati ya washindi wetu wa kila wiki aliyejishindia shilingi milioni 5 katika promosheni hii iliyobadilisha maisha ya watanzania wengi.
“Tangu promosheni ya Mimi ni Bingwa ianze katikati ya mwezi Novemba mwaka jana, tumeona watanzania wengi wakishinda kila siku na kila wiki. Airtel kupitia Airtel Money imekuwa ikihakikisha wanaojishindia zawadi za chini ya shilingi milioni 5 wanapokea pesa zao ndani ya masaa 24 bila ya kukatwa garama za kutoa, wakati wale waliojishindia shilingi milioni 5 wanapata pesa zao kupitia akaunti zao za benki,” alisema Jane.
Alisema kuwa wateja wote wa Airtel bado wananafasi ya kujishindia milioni 50 pesa taslim, kutokana na kuwa mshindi atapatikana kupitia bahati nasibu.
“Kwa mujibu wa vigezi na masharti ya promosheni, kila namba iliyojisajili kwenye promosheni, hata kama mteja amejibu swali moja tu, atakuwa ameingia kwenye droo kubwa.
“Huu ni wakati sasa wa wateja wengine wa Airtel ambao hawajajisajili kwenye promosheni waingie kwenye promosheni kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neon “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50,” alisema Jane.
Alisema kuwa washindi wa tiketi wa awamu ya kwanza ya safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford wamesharejea kutoka Uingereza na kuongeza kuwa wale wa awamu ya pili wataondika nchini hivi karibuni wakifuatiwa na wa awamu ya tatu na ya mwisho kabla ya mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.
Mara baada ya kupokea hundi yake ya shilingi milioni 5, Philemon Nathaniel Mgaya alisema pesa alizopokea zitamsaidia kutanua biashara yake aliyoianzisha baada ya kustaafu kazi katika Jeshi la Polisi.
“Ninafuraha ya pekee kuweza kushinda milioni 5 za Mimi ni Bingwa, nitazitumia pesa hizi kwa makini kwa kuongezea mtaji katika biashara yangu. Naishukuru Airtel kwa hili na napenda kuwahakikishia wateja wengine wa Airtel kuwa nao wanaweza kushinda katika promosheni hii. Nitaendelea kujibu maswali zaidi na zaidi ili nijiweke katika nafasi nzuri ya kujishindia zawadi kubwa ya shilingi milioni 50,” alisema Philemon.
No comments:
Post a Comment