Tuesday, February 18, 2014

MAN CITY HOI KWA BARCELONA, YALALA 2-0


Wachezaji wa Barcelona, Fabregas na Iniesta wakimpongeza Messi baada ya kufunga bao la kwanza.


Beki wa Man City, Martin Demichelis akimchezea Messi rafu iliyopelekea penalti na kadi nyekundu.


...Martin Demichelis akizawadiwa kadi nyekundu.


Messi akifunga bao la kwanza kwa Barcelona.

TIMU ya Barcelona imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manchester City katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester!

Mabao ya Barcelona yamewekwa kimiani na Lionel Messi kwa mkwaju wa penalti dakika ya 54 baada ya kuangushwa eneo la hatari na beki wa Man City, Martin Demichelis aliyepewa kadi nyekundu.

Bao la pili limefungwa na Dani Alves dakika ya 90 ya mchezo na kuipa ushindi wa bao 2 Barcelona.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...