Sunday, January 5, 2014

STEVE NYERERE AWA MWENYEKITI MPYA WA BONGO MOVIE




  Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
.
Makamu Mwenyekiti wa Bongo Movie,Dk Cheni akiwashukuru wadau mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama hicho

Katibu Mkuu wa Bongo Muvi,William Mtitu akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao watahakikisha chama chao kinasimama imara.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha inaendelea kukua siku hadi siku.

Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere.

 


Baadhi ya Wasanii wa Bongo Muvi wakifuatilia mchakato wa uchaguzi wa viongozi wao.

Waratibu wa Uchaguzi huo wa viongozi wa Bongo movie wakiongozwa na Mama Asha Baraka wakihesabu kura za washiriki waliongombea nafasi mbalimbali katika chama hicho.

Mratibu wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa Bongo Mov
iAsha Baraka akitoa muongozo na kuzungumza machcahe kuhusiana na uchaguzi huo.

Sehemu ya Wagombea wakisikiliza matokeo yao,William Mtitu,Steve Nyerere,Dada Wastara pamoja na Dk Cheni.


Baadhi ya Wasanii wa Bongo Muvi wakifuatilia mchakato wa uchaguzi wa viongozi wao.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...