Friday, January 24, 2014

LULU:POMBE ZILINIHARIBIA MAISHA YANGU.


MSANII wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa sasa hivi anaiogopa na kuiheshimu sana pombe akiamini kwamba ndiyo chanzo cha maisha kuharibika.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Lulu alisema tangu ametoka gerezani ameamua kujiweka pembeni na kilevi hicho na kwamba bora aitwe mshamba.
“Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo kichocheo cha kila baya hapa duniani, watakaoniona mshamba kwa kubadilika kwangu wanione hivyohivyo,” alisema Lulu. Msanii huyo kipindi cha nyuma alikuwa hakamatiki kwa kilevi na kuna wakati aliwahi kuzimika alipofakamia pombe za ofa alipokuwa ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar.
 Na Imelda Mtema

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...