Said Nassor ‘Chollo’.
BEKI wa pembeni wa Simba, Said Nassor ‘Chollo’, ataikosa mechi ya leo dhidi ya Azam kutokana na kuumia nyonga.
Simba italazimika kuivaa Azam bila nahodha wao huyo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe, amesema beki huyo aliumia katika mazoezi ya juzi kwenye Fukwe za Bamba zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Tunaangalia uwezekano wa kumpeleka hospitali leo (jana), lakini ni wazi kwamba ataukosa mchezo wa Jumatatu (leo) dhidi ya Azam,” alisema Gembe.

No comments:
Post a Comment