BAADA ya shoo ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 jijini Dar kusimama kwa muda leo alfajiri kwa hitilafu ya umeme, inatarajiwa tena kuendelea tena saa 9 alasiri leo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam bila kiingilio chochote.
Akizungumza na baadhi ya mashabiki wa tamasha hilo waliokuwepo viwanjani hapo baada ya hitilafu kurekebishwa, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alisema kuwa shoo itaendelea saa 9 mchana wa leo na wasanii ambao hawakupata fursa ya kutumbuiza kama Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' Davido kutoka Nigeria, Mohombi kutoka Sweden, Nay wa Mitego na Bendi ya Twanga Pepeta watatoa burudani ya nguvu saa 9 mchana wa leo bila kiingilio chochote kile.
Mashabiki wote ambao mlikuwa na hamu ya kuwaona baadhi ya wasanii ambao hawakutumbuiza kutokana na hitilafu ya umeme wategemee 'sapraiz' kibao wakati wa shoo hiyo. Wasanii waliopiga shoo baada ya umeme kurudi katika hali yake ni pamoja na Kalapina, Chid Benz na Darasa japo mashabiki wengi walikuwa wameondoka viwanjani hapo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo Sebastian Maganga anawaomba mashabiki wote mfike kwa wingi ili muweze kushuhudia burudani hizo.
No comments:
Post a Comment