Mbunge wa jimbo la Temeke Abbas Mtevu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliobahatika kupata ajiri ya miaka miwili Dubai,muda mfupi baada ya kuhitimisha zoezi la kuwakabidhi tiketi za kusafiria,akiwa pamoja na wadhamini wa ishu hiyo.
Mwenyekiti wa Kituo cha Bravo Job Centre, ambaye pia ni Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi Halima Selemani nyaraka mbalimbali ikiwemo tiketi ya ndege ya kwenda Dubai kufanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili, katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kituo hicho kimewatafutia wanawake watano kazi ya ndani nchini humo. Kutoka kulia ni Asmah Mshangama, Mwajuma Bakari na Fatma Saburi. Mtemvu akizungumza na wanufaika wa kazi hizo pamoja na wadhamini wao.
MBUNGE wa Temeke, Abbas Mtemvu amefanikisha wanawake watano kupata kazi nchini Dubai kwa mkataba wa miaka miwili na mshahara mnono.
Mtemvu ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Bravo Job chenye ofisi Dubai na Dar es Salaam, aliwakabidhi tiketi ya kwenda huko pamoja na nyaraka zingine muhimu ukiwemo mkataba wa kazi.
Waliofanikiwa kupata fursa hiyo ya kwenda kufanya kazi za ndani ni Halima Selemani, Fatma Saburi, Asmah Mshangama, Mwajuma Bakari walioondoka jana kwa ndege ya Qatar pamoja na Nuru Rajab aliyekwenda huko mwezi uliopita.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuwaanga, Mtemvu aliwataka watanzania hao kwenda kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu kwa lengo la kulinda heshima ya Tanzania.
Alisema kuwa endapo kama kuna mtu atakwenda kinyume,basi yeye na kituo chake wataamua kukatisha mkataba na kurudishwa haraka nyumbani.
Mtemvu alisema kuwa moja ya mambo muhimu ambayo inayafanya katika utaratibu wa kuwatafutia watu kazi nje ya nchi, ni kufuata taratibu zote za kiserikali za hapa nchini na wanakokwenda kufanya kazi.
Pia alisema kuwa kituo hicho kina utaratibu wa kwenda kuwatembelea wafanyakazi hao katika maeneo wanayofanya kazi kwa lengo la kuona kama wanatendewa vizuri na waajiri wao.
Alitaja fursa zingine za kazi zinazopatikana katika nchi za Falme za Kiarabu kuwa ni udereva teksi, ujenzi, upakaji ina na uhasibu na uselemala.
Wanawake hao, waliimpongeza Mtemvu na kituo chake kwa kubuni utaratibu huo na
kuwawezesha kupata kazi, jambo ambalo hawakutarajia katika maisha yao kwamba wanaweza kupata kazi nje ya nchi.Pia waliahidi kutokiuka makubaliano ya mkataba wao.
Kupitia kituo hicho, Mtemvu ameahidi kuwatafutia kazi watanzania katika nchi za Falme za Kiarabu na kwingineko duniani, ili kuipunguzia Serikali tatizo la ajira.
No comments:
Post a Comment