Tuesday, October 22, 2013

MAKAMU WA RAIS AONGOZA SHUGHULI ZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU JULIUS NYAISANGA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Gharib Mohamed Bilal,akiongoza safu ya Watanzania kwenye shughuli za kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji mahili wa vituo mbalimbali vya redio na TV, Uncle Julius Nyaisanga kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, mapema leo baada ya kupoteza maisha juzi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambapo alikuwa akiishi na kufanyia kazi yake ya Utangazaji kwenye kituo cha redio na TV ya Abood.

Gari Maalum lililobeba Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle J),likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam tayari kwa zoezi la kuaga Mwili huo ambao utasafirishwa kwenda Kijijini kwao Tarime,mkoani Mara kwa Mazishi.Marehemu Julius Nyaisangah alikuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD) yeye pamoja na Mikidadi Mahmoud mwanzoni mwa miaka ya 90. Waanzilishi wengine ni Aboubakary Liongo, Rankim Ramadhan, Flora Nducha,Vicky Msina,Taji Liundi,Charles Hillary na Blandina Munghezi.Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali hapa nchini wakishirikiana kwa pamoja kubeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle J) ulipowasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo.

Mmoja wa Wanahabari waliowahi kufanya kazi na Marehemu Julius Nyaisangah,Dkt. Misanya Bingi akiwa amebeba msalaba wenye jina la Marehemu.

Mwili ukihifadhiwa sehemu iliyoandaliwa. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).Marehemu Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...