Waziri Mkuu wa Tanzania
Mizengo Pinda (katikati), akiitembeza na kuionyesha timu ya Serengeti Fiesta
baadhi ya vitu vinavyofanyika shambani hapo.
TIMU ya Serengeti Fiesta hususani iliyoupande wa kampeni ya
Kamata Fursa Twenzetu, mapema leo ilipata mwaliko kutoka kwa Waziri Mkuu wa
Tanzania Mh.Mizengo Peter Pinda wa kutembelea katika mashaba yake.
Timu hiyo ilifika kwenye mashamba hayo yaliyopo Kizoto nje
kidogo ya mji wa Dodoma eneo la Zuzu ambalo ndilo jina halisi la mashamba hayo
ambayo yanafanyika vilimo mbalimbali, ikiwemo ufugaji wa Mbuzi zaidi ya mia
mbili,kilimo cha Zabibu,Nyanya,Ndizi na ufugaji wa asali.
Timu hiyo ya Clouds Group ilikuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa
Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group Rugemalila Mtahaba ‘Ruge’, ilipata
fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Waziri Mkuu,hasa kuhusiana na
namna ya kutumia fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia kilimo na ufugaji.
Waziri Mkuu akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa
Vipindi,Uzalishaji na Maendeleo wa Clouds Group Ruge Mtahaba (kulia), moja ya
mikakati yake ya baadae atakayoifanya shambani hapo.
Mtalamu na msimamizi Mkuu wa mashamba hayo aliyeshika chupa
(kushoto), akionyesha moja ya chupa ya asali inayotengenezwa hapo.
Mtalamu wa mashamba hayo
akiwatembeza na kuwapa maelezo na jinsi walivyoweza kufanikisha kilimo na
ufugaji huo.
Moja ya Shamba la Zabibu likiwa katika muonekano wake.
Shamba la Nyanya
likionekana.
Moja ya mabanda ya mizinga
ya nyuki.
Mwandishi wa Kampuni ya
Global Publishers LTD Musa Mateja (kushoto), akipeana mkono wa pongezi na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Ruge akiwa katika Pozi na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mtangazaji wa Kipindi cha Amplifier Millard Ayo akiwa katika
pozi na Waziri Mkuu.
Mateja akiwa katika pozi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi Wasiwasi Mwabulambo (kulia),
akipokea zawadi ya Zabibu kutoka kwa Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment