Sunday, September 15, 2013

SERENGETI FIESTA KAMATA FURSA YAWAFIKIA VILIVYO WAKAZI WA MOROGORO

 Mkurugenzi wa Vipindi na Maendeleo wa Clouds Group Ruge Mtahaba, akijaribu naye kutumia uzowefu wake kwa kuwaonyesha wakazi wa Morogoro namna ya kutumia Fursa zilizopo mkoani hapo.

SEMINA ya Kamata Fursa Twenzetu inayotolewa na timu ya Serengeti Fiesta 2013, kila mkoa inapotua burudani hiyo, leo imeendelea tena kujenga na kupanua mawazo ya wakazi wa Morogoro katika mpango wa kuwawezesha kujua namna ya kutumia fursa zilizopo mkoani hapo katika kujikwamua kwenye maisha yao.
Semina hiyo ilifanyika mapema leo katika Ukumbi uliopo katika Hoteli ya Midland mjini Morogoro, ambapo baadhi ya wataalam kutoka sehemu mbalimbali walipata muda wa kuzungumza na wakazi hao na kuwajenga kwa kuwaonyesha njia mbalimbali za kujikwamua kimaisha.

Baadhi ya wakazi wa Morogoro waliokuwa wamehudhuria ukumbini hapo wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
Meneja wa ujasiliamali wa Zantel Haidar Chamshama,akiwaonyesha wakazi wa Morogoro namna ya kutumia fursa ya kubana matumizi kwa upande wa utumiaji wa simu za mkononi na kujua faida za simu zaidi katika kujikwamua kimaisha.

Mkuu wa maswala ya utafiti wa Maxcom Africa Ahmed S Lussasi, akiwafafnulia wakazi wa Morogoro namna wanavyoweza kufaidika na bidhaa za Maxcom katika kujikwamua kimaisha.

Mtangazaji wa Kipindi cha Sport Extra cha Clouds FM,Shaffi Dauda akionyesha namna ya kutumia  fursa kwa upande wa michezo.

Mbunifu wa Mavazi wa Morogoro,Diana Magesa (kushoto),akizungumzia fursa ya mambo ya ubunifu,huku akionyesha na mavazi yake kwa kumvisha Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Jerald Hando, ambaye alikuwa mshereheshaji wa semina hiyo. 

Mwakilishi wa NSSF kutoka Makao Makuu, Salim Khalifani akizungumzia namna ya kutumia fursa zinazotokana na mafao ya NSSF kwa wakazi wa Morogoro leo ndani ya Ukumbi wa Midland Hoteli mjini Morogoro.

 Ruge akihitimisha Semina hiyo kwa kukaribisha maswali kutokana na mafunzo waliyoyapata wakazi wa Morogoro walihudhuria kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu mapema leo.

Baadhi ya wakazi waliokuwa ndani ya ukumbi huo wakiwa wamesimama baada ya kuombwa kuimba wimbo wa Tanzania na Mrisho Mpoto kabla ya kuanza kuonyesha fursa kupitia sanaa yake ya Muziki wa Kughani Mashairi.

Msanii wa Kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwaimbisha wimbo wa Tanzania wakazi wa Morogoro muda mfupi kabla ya kuanza kutoa njia za kutumia fursa kupitia sanaa ya muziki.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...