Monday, July 22, 2013

JOHN MNYIKA ANUSURIKA BOMU



Mbunge wa Ubungo, John Mnyika jana alinusurika kupigwa na bomu la machozi lililorushwa na polisi waliokuwa wakizuia kufanyika mkutano ulioitishwa na chama hicho.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la Mabibo kwenye viwanja vya Sahara ambapo bomu hilo lilimpata mtu aliyekuwa karibu na Mnyika anayeitwa Thomas Jerome, aliyejeruhiwa sehemu ya paja.

Baada ya kurushwa kwa bomu hilo, polisi walitaka kumchukua majeruhi huyo ili wamweke kwenye gari lao apelekwe hospitalini, lakini Mnyika aliwaelekeza wafuasi wa CHADEMA kumchukua kwa madai kitendo kilichofanywa na askari hao kililenga kuficha ushahidi wa jambo hilo.

Polisi waliokuwemo eneo la tukio waliamua kukubaliana na matakwa ya wafuasi wa CHADEMA waliomchukua Jerome na kumpeleka hospitali ambako hali yake inadaiwa inaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...