Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Steven JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.
Pazia la Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbalawa
Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji
Msanii Steve Nyerere akipokea Tuzo
Msanii Nice Mohamedi ‘Mtunis’ akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entertainment
MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI
Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake
Riyama akipokea tuzo yake
Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabizi tuzo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi ‘Ray ‘ wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana usiku.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos ‘Ray’ ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo
Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizodhaminiwa na kampuni ya steps.
MPIGA PICHA MOHAMED ARALAKIA ZA COVERS MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO
KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo
Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo
Baadhi ya washindi ambao waliopatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Steven Mangendela ‘Steve Nyerere’, Issa Mussa ‘Cloud 112′ Mohamed Nurdini ‘Chek budi’ Nice Mohamed ‘Mtunisi’ Irene Paul akinyakuwa msanii bora chipukizi wa kike
Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Steven ‘JB’ huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Irene Uwoya, na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda ‘Jimmy Masta’
Wakati katika kipengele cha muongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi’ Ray’ na kampuni yake ya RJ Filamu
Mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri lakini kwa sasa hawapo duniani moja ni kwa Steven Kanumba, Juma Saidi Kilowoko ‘Sajuki’ John Stefano, Hussein Ramadhani Mkiety ‘Sharo Milionea’
Katika utoaji wa tuzo hizo kulikuwa na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi
No comments:
Post a Comment