Monday, June 17, 2013

AIRTEL YATOSHA YAINGIA MTAANI KWA MBWEMBWE!!!


Wafanyakazi wa Airtel wakiwa wameshikana mikono kama ilivyo katika tangazo lao la gazeti na televisheni kuashiria kuwa huduma ya Airtel Yatosha kifurushi cha SIKU imeboreshwa na sasa ni masaa 25, ishara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye barabara ya Old Bagamoyo. Aliyevalia kijamii ya Maasai ni Bw. Petro Abraham Lucas ambaye ni muhamasishaji wa huduma ya Airtel Yatosha.
Wafanyakazi wa Airtel Kitengo cha huduma kwa wateja wakiongozwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa kwanza Bi. Adriana Liamba kushikana mikono kuashiria kuboreshwa na kuitambulisha rasmi huduma yao ya Airtel Yatosha kwa wateja ambayo sasa imeboreshwa zaidi ili kumuongezea mteja muda zaidi wa kutumia kifurushi chake cha siku kwa masaa 25 toka alipojiunga.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara mpya cha Airtel Bw, Godfrey Mugambi akiwa na wafanyakazi wenzake wakiwa wameshikana mikono kuonyesha kweli Airtel Yatosha.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania makao makuu Dar es Salaam wakiingia barabarani huku wameshikana mikono kwa maandamano ikiwa ni tukio maalum la kuitambulisha TOSHA 24+1=25.
Wafanyakazi wa Airtel toka vitengo mbalimbali wakiwa wamejipanga na kushikana mikono kuashiria kuboreshwa kwa huduma yao ya Airtel Yatosha kwa wateja ambayo sasa imeboreshwa zaidi ili kumuongezea mteja muda zaidi wa kutumia kifurushi chake cha siku kwa masaa 25 toka alipojiunga. Ili mteja kujiunga anatakiwa kupiga *149*99# , tukio hili lilifanyika mwishoni mwa wiki katika barabara ya Old Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...