Tuesday, April 9, 2013

VURUGU NA MIGOGORO YASABABISHA MAJENGO MATATU YA SHULE YA SEKONDARI YA IFUNDA KUCHOMWA MOTO



Majengo matatu ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, mkoani Iringa yamechomwa moto kwa siku tatu mfufulizo na kuteketea kabisa, huku chanzo cha matukio hayo kikitajwa kuwa ni hujuma kutokana na mgogoro uliopo shuleni hapo.


Shule hiyo ya mchepuo wa sayansi ambayo ilianzishwa mwaka 1950, imeingia katika migogoro baina ya uongozi wa shule hiyo na wafanyakazi na baadhi ya wanafunzi.

Wanafunzi 10 walisimamishwa hivi karibuni 10 kutokana na utovu wa nidhamu, hatima yao inasubiri kikao cha bodi ya shule Aprili 17, mwaka huu.

Wakati wanafunzi hao wakiwa wamesimamishwa, walimu watatu wamepewa barua za uhamisho ikitajwa kama sehemu ya kuboresha ikama ya ualimu shuleni hapo.

Kaimu mkuu wa shule hiyo, Twaha Mruma alimweleza Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Gerald Guninita aliyefika shuleni hapo jana kujionea kiwango cha uharibifu huo kuwa, matukio ya kuchomwa moto majengo hayo ni hujuma. Alisema matukio hayo yalianza Mwezi Aprili 4, mwaka huu na yamefanywa kwa siku tatu mfulululizo

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...