Monday, April 8, 2013

Fid Q, Ney Wamitego wafunika Tamasha la Airtel YATOSHA COCO Beach Jana,





Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda maarufu kama Fid Q akitumbuiza wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki
Airtel Tanzania imeendeleza ahadi yake ya kuzunguka nchi nzima kutoa elimu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla ili kuifahamu huduma yao ya AIRTEL YATOSHA pamoja na faida zake

Dokezo lilitolewa na meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema "tunawashukuru sana watanzania wote waliojitokeza Coco beach nakujiunga na huduma yetu nafuu ya Airtel yatosha, wote wameikubali na wameona ukweli wa mambo kwamba kweli Airtel yatosha nyingine ya nini???

Tuwape mpya ya wiki hii ni kwamba tunahamia zetu chalinze, wateja wetu wa mkoa wa pwani sasa ni zamu yenu kupata burudani na elimu ya faida zilizopo ndani ya hii AIRTEL YATOSHA, tutapiga kambi kwa siku mbili yaani Juma mosi na Jumapili paleee kwenye viwanja vya sokoni Chalinze na wasanii kibao na zawadi kibao zitakuwepo

Ni wazi kuwa hii haina kiingilio njoo wewe na mshikaji wako upate burudani na ujifunze kutumia huduma yetu mpya ya Airtel yatosha ambayo ni rahisi kujiunga na kujipatia zawadi ofa kibao ukiunga kwa kupiga *149*99# KISHA utaweza kupata dakika za BURE, Intaneti pamoja na SMS zako za kutuma kwenda mtandao wowote nchini

Wasanii watakaotumbuiza chalinze mwishoni mwa wiki hii ni Fid Q, Juma Nature na wanaume Halisi, Madee na kundi zima la Tip top Connection, pamoja na Ney wa Mitego anaetambasana katika miondoko ya Hip Hop.




MC shabani Rugage aka Kidevu cha kuku na MC Aloyce aka Adam wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki



Kundi la sarakasi la la jijini Dar es salaam likitoa burdani kwa maelfu ya watanzania waliohudhuria tamasha la Airtel Yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki



Kundi la Kinoko........ likitoa burudani wakati wa wa Tamasha la Airtel yatosha Yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki



Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda maarufu kama Fid Q akitumbuiza wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki



Umati wa watu waliohudhuria tamasha la Airtel yatosha jijini Dar es saalam wakipata burudani huku wakishika mabango ya kuwashangilia wasanii mahiri wa kizazi kipya katika tamasha la Airtel yatosha Fid Q alionekana kung'ara zaidi



Msanii wa kundi la Tip top connection Tunda man akitoa burudani kwa wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki



Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi akibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki



Msanii wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop maarufu kama Ney wa Mitego akimwaga burudani kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki



Mkuu wa Majaji (JB) aliyemiliki jukwaan na msanii nguli wa bongo fleva Sir, Juma Nature (hayupo pichani) akitoa burdani wakati tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki



Msanii maarufu wa kizazi kipya Sir Juma Nature akimwaga burudani katika tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki



Msaninii maarufu wa Hip Hop Roma Mkatoliki akiwapagaisha wapenzi wake katika tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki













No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...