Wednesday, April 17, 2013

PENNY WA DIAMOND ATOA MSAMAHA KWA PLATNUM..SAKATA LA UWOYA



Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamua kutulia na mpenzi mmoja, mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa, hivi karibuni staa huyo ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya.....

Magazeti ya udaku nchini yaliandika habari hiyo ikiwa na picha inazowaoenesha mastaa hao wakichukua chumba kwenye hoteli ambako walienda kufanya yao.

Kufuatia tetesi hizo, mwandishi wetu amezungumza na mpenzi wa sasa wa Diamond, Penny ambaye amesema kwa ufupi kuwa wameshayazungumza na Diamond na wako vizuri kwa sasa lakini akasisitiza kuwa asingependa kuliongelea zaidi suala hilo.

Katia hatua nyingine, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Diamond amekanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la udaku kuwa amemcheka Irene kwa kunaswa kwenye himaya ya Diamond.

“Mimi hivyo vitu havinihusu na wanapenda kupata quotes zangu pasipo hitajika. I don’t know why? I don’t why wanatafuta story. That’s their life kiukweli with whatever they choose to do, more power to them,” amesema

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...