Wednesday, March 20, 2013

NEY WA MITEGO AMEWACHA WASANII WENZAKE WANAO DIS NGOMA YAKE MPYA NA DIAMOND.


Mwana muziki ambae anafanya poa sana kwenye game ya Bongo fleva hapa nchini Tanzania muite Ney wa mitego a.k.a True boy leo ameamua kufunguka kwa wasanii wenzake ambao wametokea kudis wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Diamond unaitwa "Muziki Gani" Ney amewachana hiviii
"Najua ni kwanini wanasema hivyo mimi huwa naongea ukweli siku zote, wana hip hop sikuzote ni wanafiki na wanamajungu, iko hivyo na ndiyo wasanii siku zote wako na shida hawana maendeleo.

kwa sababu ya majungu yao, mimi sitaki kubishananao kwanza najua hawajielewi, hawajui huu ni muziki na hii ni biashara, mwisho wa siku mtu ambae upeo wake ni mfupi kiasi hicho inabidi tuachanenae,

Wasanii wa Hip hop hivyo na wao ndo wamejenga matabaka ya Bongo fleva na Hip hop, kwa sababu muziki wetu ulikuwa ni Bongo fleva, wooote ni Bongo fleva haijalishi huu ukiwa unaiba, huu ni wanini mladi ukiwa unatumia tu kiswahili ni wa bongo fleva, angalia hao wasanii wanobisha wako na maisha gani wako na maendeleo gani, soo me sina time nao wajipange tuu" alisema Ney wamitego.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...