Filamu ya Ray of Hope iliyoshinda tuzo za Africa Magic.
Filamu ya Kitanzania ijulikanayo kwa jina la “The Ray of Hope” iliyotengenezwa na kampuni ya Pilipili Entertainment imeshinda tuzo ya filamu bora iliyotumia lugha asili ya Kiswahili katika tamasha la Tuzo za Watazamaji wa Afrika Magic “Africa Magic Viewer’s Award.”
.
Pastor Myamba mmoja ya washiriki filamu ya Ray of Hope.
Joyce Fisoo Katibu wa Bodi ya Filamu alikuwa jaji katika tuzo hizo.
Akizungumza wakati wa mahojiano jana jijini Dar es salaam Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Bi.Joyce Fissoo amesema ushindi wa tuzo hiyo ni Heshima kwa nchi na inatoa hamasa kwa waigizaji wa filamu nchi.
“Tuzo hii ni heshima kwa nchi kwa sababu inaonyesha filamu zetu zinaweza kufikia kiwango cha kimataifa,na filamu zote zilikuwa zimekaguliwa nakupewa madaraja.”Alisema Bi. Fissoo.
Aidha Bi.Fissoo amesema tuzo hizo ni changamoto kwa wasanii na watengeneza filamu nchini kutumia fursa zinazojitokeza kushiriki katika matamasha makubwa na tuzo mbalimbali za kimataifa ili kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine jinsi wanavyoweza kutengeneza filamu zenye ubora.
.
Filamu ya Ray of hope iliyoshinda tuzo.
Hashim Kambi mshiriki katika filamu ya Ray of Hope iliyoshinda tuzo.
Tuzo hizo zilifanyika hivi karibuni jijini Lagos, nchini Nigeria ambapo filamu 110 zilizotengenezwa na makampuni 43 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ziliingia kwenye kinyanganyiro na tuzo 28 zilitolewa kutoka makundi 26.
Aidha filamu hizo zilikaguliwa na majaji tisa kutoka nchi za Ghana, Cameroon, Kenya ,Nigeria, Afrika kusini, Uganda na Zambia pamoja na Tanzania iliyowakilishwa na Katibu wa bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo.
Bi Fissoo amesema Tuzo hizo ni za kwanza kufanyika na zilifunguliwa na Waziri wa Gesi na Mafuta wa nchini Nigeria aliyemwakilisha rais Goodluck Jonathan ,viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji na Waziri wa Utamaduni na Utalii.
Vilevile tuzo hizo zilipambwa na bendi za muziki na waimbaji mbalimbali kama Femi Kuti, Tiwa Savage , Iyanya pamoja na kundi la Sauti Soul kutoka Kenya.
No comments:
Post a Comment