Thursday, February 7, 2013

"VITAMBULISHO VYA TAIFA KUTUMIKA KATIKA UCHAGUZI UJAO"....KIKWETE

RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amehaidi kuwasaidia Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kwa kuiwezesha kupata fedha kwa ajili Vitambulisho vya Taifa ili kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 watu wote watakuwa na vitambulisho vya Taifa vitakavyo tumika katika uchaguzi huo.

Aidha Rais Kikwete aliitaka NIDA kutoa vitambulisho kwa watu wanaotakiwa na kuchukulia hatua za kisheria wale watakaokiuka sheria ya usajili wa vitambulisho hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Rais Kikwete wakati uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete aliwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa zao kwa uaminifu na kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi hilo.

Aliwataka viongozi wa dini, serikali na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano huo.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi alisema ni muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya usajili ya kitaifa.

Baadhi ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo wa vizazi na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI, Mifumo ya mawasiliano yasimu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan Board),n.k.


Mkurugezi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.


Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni vifaa vya kuchukulia alama za vidole, picha saini takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili kukukamilisha mpango huo kwa muda utaotakiwa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...