Omotola na mume wake watatu kutoka kushoto wakiwa na familia yao mwaka 2012.
-------------
Baada ya kuingia kwenye headlines na kukanusha kwamba hajafanyiwa opareshen ya kuondoa nyama zilizozidi tumboni kwake, mwigizaji Mnigeria Omotola Jalade ambae amewahi kuja bongo kuzindua movie mpya ya Wema Sepetu, ameingia tena kwenye headlines.
Sasa hivi amehusishwa na taarifa za kuaminika kwamba amekua akimpiga mumewe aitwae Mathew Ekeinde, na hiyo hutokea mara kwa mara pale wanapokosana.
Stori inaendelea kutiririsha kwamba pamoja na tabia hiyo aliyonayo Omotola, Ekeinde amekua mvulivu na mwenye busara na amejizuia sana manake hajawahi kumpiga hata siku moja kwa sababu anampenda sana.
Omotola kweli anahulka ya kibabe, nakumbuka wakati alipokuja bongo nilipata nafasi ya kuingia kwenye chumba chake alichokua analala, nilikwenda kumfanyia interview… nilishuhudia jinsi alivyokua akimuendesha Cameraman wake kibabe, pia alimzodoa kibabe mbele ya watu kijana mmoja ambae alimkubalia kupiga picha lakini kijana akamshika Omotola kiunoni, ghafla mwigizaji huyo akabadilika na kumuwakia kwamba asimfananishe na madem wa saizi yake, hatakiwi kumshika hivyo.
No comments:
Post a Comment