Saturday, February 23, 2013

MIMBA YA SISTER P YAYEYUKA...!






MIMBA ya msanii wa hiphop hapa Bongo, Happy Peter maarufu kama Sister P, imeyeyuka kufuatia mazoezi makali ya kujiandaa na wimbo wake mpya.
Akiongea katika ofisi za Saluti5 jana jioni, Sister P aliyetamba enzi hizo na kibao chake “Anakuja”, alisema anasikitika kuwa mimba yake imeharibika.
“Nilikuwa nafanya mazoezi makali ya kukimbia ufukweni pamoja na kuingia gym ili nipate stamina ya kupasuka vizuri kwenye ‘mic’ kumbe nilikuwa nauweka rehani ujauzito wangu.
“Siku moja baada ya kutoka mazoezini nikaenda studio kuingiza sauti, wakati naendelea kufanya makamuzi nikapatwa na maumivu makali ya tumbo.
“Nikakimbizwa hospitali na baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa mimba imeharibika” alisema Sister P msanii msela kupindukia kiasi cha kufanya watu wapate utata juu ya jinsia yake.

Sister P amesema wimbo wake mpya uliosababisha kupoteza ujauzito wake umeshakamilika na hivi punde atauachia hewani. Hivi karibuni gazeti moja liliandika juu ya ujauzito wa Sister P na kuzua mshtuko mkubwa wengi wao wakiwa hawaamini kama msanii huyo ana bwana achilia mbali kuwa na mimba

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...