MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolper anaamini mafanikio hutokana na juhudi, kujituma pamoja na kutimiza malengo yako uliyojiwekea kwa kipindi ulichokusudia
Msanii huyo wa filamu alielezea maisha yake yako nje ya Tasnia ya filamu alipokutana na mwandishi wa safu hii
Wolper mbali na kuigiza pia yeye ni mcheza netiboli katika timu ya bongo movi akiwa anachukua nafasi ya mfungaji 'GS' huku akiwa tishio kwa timu pinzania kwa uwezo alionao na jinsi anavyoweza kutumia urefu aliokuwa nao kwa kufunga magoli mengi
Alianza kucheza netball akiwa shuleni na huko ndipo alipopata ujuzi wa mchezo huo ambapo mpaka sasa ameweza kuwa tishio kwa kuumudu mchezo huo na kuweza kuisababishia ushindi kwa timu anayoichezea
Alisema kuwa anapata muda wa kutosha kufanya mazoezi kila siku jioni na asubuhi hivyo mazoezi yanamsaidia kujenga mwili wake pia na kumpa pumzi zinazomsaidia kucheza kipindi chote bila ya kupumzika mpaka mwisho wa mchezo
Aliendelea kusema kuwa kwa upande wake anathamini sana mazoezi kwani yanamfanya kuzidi kuwa imara na pia hutumia mazoezi kwake ni kama dawa ya kuondoa uchovu katika mwili wake
Wolpa aliweka wazi kuwa kama ingekuwa si muigizaji basi angekuwa mchezaji mzuri wa netball na angeongeza nguvu katika hilo na kuweza kuchezea timu kubwa na anaamini kuwa angefanya vizuri kwenye upande huo
Anaeleza kuwa hatoweza kusahau siku alipoumia vidole vya mikono kwenye mechi iliyokuwa inachezwa katika viwanja vya Leaders Club na aliweza kuendelea kucheza mchezo huo na hatimaye waliibuka washindi katika mechi ya kujipima
Mbali na kucheza netball pia msanii huyo ni bingwa wa kuogelea, huku akidai kuwa muda wake mwingi wa mapumziko anautumia kuogelea ili kuweka mwili wake imara
Aliongezea kuwa mara nyingi huwa anaratiba ya nini afanye muda gani na kipi kifanyike wakati gani hiyo ndiyo moja ya kitu anachoamini kuwa kinampa mafanikio makubwa katika maisha yake
Wolper alisema huwa hapendi kuwa na makundi ya watu hivyo hawezi kuamua kwenda kukaa bar kama hana kazi ya kufanya kwa sababu ratiba yake inakuwa imejaa muda wote ule
Wolpera ambaye pia alikuwa anafanya biashara ingawa sasa anajipanga kuianzisha tena biashara yake ili maisha yake yaendelee kuwa yenye mafanikio kwa juhudu anazozifanya
Aliongezea kuwa anapenda kusoma vitabu muda wa mapumziko zaidi kuliko kwenda kukaa bar na marafiki ambao kwake anahisi labda hawana mafanikio ingawa si kila rafiki ni mwema au ni mbaya hivyo kwa upeo wa kiubinadamu huwezi kutambua hilo kwa haraka
Anasema kuwa kusoma vitabu kunamsaidia kumjenga kiuwezo na fikira pia inamuongezea kuwa mbunifu hususani katika kazi zake za sanaa
Wolper ni msanii wa filamu ambapo alianza kuigiza mwaka 2009 na filamu iliyomtambulisha ni Amazangu amazao kwa sasa anatamba na filamu nyingi ikiwemo ya Ndoa yangu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba
No comments:
Post a Comment