Akina mama wakilia baada ya kifo cha ghafla cha Padri Evarist Mushi kilichotokea jana asubuhi kwa kupigwa risasi muda mfupi kabla ya kuanza misa ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki la Kigango cha Mtoni, Zanzibar.
PADRI wa
Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili lililoko Mji Mkongwe Zanzibar,
Evaristus Mushi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana
asubuhi wakati akielekea kanisani kuendesha ibada.
Tukio hilo limetokea majira ya saa moja asubuhi wakati padri huyo akijitayarisha kwenda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtoni nje kidogo na Mji wa Zanzibar.
Hilo ni tukio la pili kutokea kwa padri kupigwa risasi Zanzibar baada ya Desemba 26, mwaka jana Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki, Mjini Zanzibar kupigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake saa 1:45 jioni wakati akitokea kanisani.
Akizungumzia tukio la jana, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema pamoja na kuthibitisha, alisema ametuma timu ya wapelelezi kwenda Zanzibar kuchunguza kwa undani kuhusu tukio hilo.
“Watu wasiojulikana wamempiga risasi Padri Mushi, na baada ya tukio alipelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kufariki dunia. Polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,” alisema IGP Mwema.
Alisema hadi sasa watu watatu wameshakamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea na kuchunguza tukio zima.
IGP Mwema alisema ametuma timu Zanzibar itakayoongozwa na Manaibu Kamishna wa Polisi wawili ambao ni Samson Kasalla na Peter Kivuyo wakiwa pamoja na Kamanda wa Operesheni wa jeshi hilo, Simon Sirro.
“Tumekuwa tukifuatilia nyendo hizi na hivi sasa tutapambana na wahalifu ipasavyo, vurugu zozote zile lazima tupambane nazo ipasavyo,” alisema Mwema na kuongeza: “Kama kwenye tukio hili kutakuwa na masuala ya kigaidi nayo tutachunguza.”
Alisema watawatafuta kwa udi na uvumba wale wote wanaochochea au kufadhili yanayotokea kwa kuwa wanachokifanya ni uhalifu.
Mwili wa padri huyo sasa umehifadhiwa katika mochwari ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Katika Kanisa la Minara Miwili, Mji Mkongwe waumini walikusanyika wakionyesha hali ya kuchanganyikiwa baada ya kupata taarifa za kifo hicho cha ghafla.
Wakizungumza kwa masikitiko waumini hao wamesema hawakuwa wakijua chochote kilichotokea hadi hapo walipofika katika kanisa kwa ajili ya kufanya ibada.
“Tumetoka nyumbani tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya ibada zetu kwa amani, lakini tulipofika hapa tumepokea taarifa.
kuwa padri wetu amepigwa risasi, jamani Mungu hiki ni nini, mbona Zanzibar imegeuka kuwa nchi isiyo na amani, vipi tutaishi katika hali kama hii ya kuhofu na wasiwasi...Mungu tusaidie waja wako sisi,” alisema mama mmoja huku akilia kwa majonzi.”
Mashuhuda.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema kawaida Padri Mushi huwa anakwenda kusalisha katika Kanisa la Mtoni na kwamba jana, baada ya kufika kanisani hapo wakati akitaka kuegesha gari lake walifika watu kwenye gari lake na kumfyatulia risasi na kisha kukimbia kusikojulikana.
Makamu Askofu wa kanisa hilo Zanzibar, John Mfoi alisema kuwa watu waliompiga risasi Padri Mushi walikuwa wapo kwenye pikipiki aina ya Vespa na walikuwa wakimfuatilia kwa nyuma wakati akieleke kanisani.
“Baada ya kufika karibu na kanisa alipigwa risasi na gari kupoteza mwelekeo kisha kwenda kuonga nyumba,”alisema na kuongeza:
“Uchunguzi wa hospitali umegundua alipigwa risasi tatu mbili zimetolewa kichwani na nyingine haijulikani iliko.”
Matukio kama hayo ya kihalifu yamekuwa yakitokea mara kwa mara Zanzibar ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja watu watatu walipigwa risasi maeneo ya Bububu na Mbweni, lakini hii ni mara ya pili kwa padri kupigwa risasi katika historia ya Zanzibar.
TEC wasikitika
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Severin Niwemugizi alisema tukio hilo linatia mashaka kwa kuwa mauaji hayo yanaonyesha kuwa ni ya kupanga.
“Nimepata taarifa kwamba kuna mwenzetu ameuawa huko, lakini inaonekana ni mauaji ya kupangwa kwa kadiri ya hamasa ambazo zinatolewa na dini fulani, kwani waliwahi kusema hatutaifurahia Pasaka, nadhani ndiyo wanatekeleza hilo,” alisema Niwemugizi.
Alisema tukio hilo ni la kuogopesha na linaonyesha nchi inakoelekea si kuzuri kwa kuwa kikundi fulani kimeachiwa na kinafanya mauaji na kuwatendea maovu wengine lakini viongozi wamekaa kimya.
“Hii ni ishara mbaya kwani Serikali ipo hivyo tunahitaji kauli yao kuhusu haya mambo, kwa kweli nina mashaka na yanayotokea ili yasije yakatufikisha kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda,”alisema Niwemugizi.
JK atuma rambirambi
Rais Jakaya Kikwete alisema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Mushi.
“Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”

Gari alilokuwa anaendesha Padri Evaristus Mushi baada ya kupigwa risasi na kupoteza maisha.
Padri Evaristus Mushi.
No comments:
Post a Comment