Thursday, January 10, 2013

WEZI WAMLIZA MH. TEMBA KWA MARA NYINGINE.



Ikiwa imepita miezi miwili tu tangu wezi waifanyie kitu mbaya gari ya Mheshimiwa Temba aina ya Verossa, kwa mara nyingine tena wezi wameiba vifaa vya gari lake.
Taarifa hiyo imetolewa na leo na Chege kupitia Twitter ambaye ameandika:

Wazee wa power window mtuhurumie!watu hata bila huruma wamemuibia tena vitu vya gari temba,lkn mwisho wa mchezo huu hautokua mzuri ni lawama.

Mwishoni mwa mwaka uliopita watu wasiojulikana waliiba vifaa vya gari lake wakati lilipokuwa limeegeshwa nyumbani kwake.

Vifaa vilivyoibiwa katika tukio la kwanza ni pamoja na power window, side mirror zote taa za nyuma, radio leseni hadi madaftari yake ya shule.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...