Thursday, January 10, 2013

MAKAHABA 22 YANASWA NA JESHI LA POLISI...BEI ZAO ZILIKUWA NI SH. 2000 TU!


Jeshi la Polisi Tanzania limewakamata zaidi ya wasichana wapatao 22 eneo la Mwananyamala karibu na geti la Mwananyamala hospitali akiwemo mama mtu mzima anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 ambaye alikuwa anamiliki jumba lenye zaidi ya vyumba 40 ambalo utumika kufanyia ukahaba maarufu kama danguro.
Akitoa taarifa leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamanda Charles Kenyela, alisema kuwa wanashukuru wananchi ambao wameweza kutoa ushirikiano wa kukamatwa kwa wasichana hao ambao walikuwa wakifanya biashara ya ukahaba katika maeneo hayo kwa muda mrefu.

Mashuhuda wa tukio hilo, walisema kuwa wanalishukuru sana Jeshi Polisi kwa kuweza kuwakamata wasichana hao ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo ya ukahaba kwa muda mrefu.

"Tunalishukuru sana Jeshi la polisi kwa kuvunja kero hii ambayo imekuwa ikitukera tokea muda mrefu sana, yani danguro hili lipo tokea mwaka 1990, mimi nazaliwa nalikuta mpaka leo lipo ila leo ndiyo polisi wamekuja kuwakamata wahusika" Alisema mmoja ya vijana wanaoishi eneo hilo.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa wanafanya biashara hiyo kwa bei ya shilingi 2000, 3000 kwa muda mfupi (short time) na wateja wao ni vijana, akina baba pamoja na vijana ambao huwa wanabarehe kwa vile hawa huwa hawajui mapenzi huko huenda kufundishwa




No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...