Tuesday, January 8, 2013

OMARI OMARI HATUNAYE TENA....

 
 Marehemu Omar Omar enzi za uhai wake.
WAOMBOLEZAJI mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, leo wamekusanyika nyumbani kwa mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya mnanda, Omar Omar Mfungilo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao Temeke-Mikoroshini, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa baba mdogo wa marehemu, mzee Yusufu Ally Mfungilo, marehemu Omar anatarajiwa kuzikwa kesho saa saba mchana huko Temeke.
 
Ndugu na jamaa wakiwa na majonzi msibani kwa marehemu Omar Omar, Temeke-Mikoroshini jijini Dar.
 
Dada wa marehemu (hakufahamika jina lake mara moja) akiwasiliana na ndugu wengine ambao hawapo msibani.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, mwenye T-shirt ya mistari (nyuma katikati) akibadilishana mawazo na wazee msibani hapo.

 
Meneja wa marehemu, Bonga Ticha (kushoto) akiwa na meneja wa kundi la muziki la Wanaume Family, Mkubwa Fella.
 
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na mameneja wao wakiwa msibani hapo.





No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...