Wednesday, January 9, 2013

MZEE MAGALI ATOA YA MOYONI KUHUSU WASANII WA KIUME WANAOJICHUBUA



MSANII nguli wa filamu za Kibongo, Charles Magali ‘mzee Magali’ amesema kuwa anachukizwa na tabia ya baadhi ya wasanii wa kiume wa filamu wanaojichubua na kuweka dawa nywele zao.

Akizungumza na na mwandishi wa habari hii, mzee Magali alisema kwa muda mrefu amekuwa akilikemea jambo hilo bila ya mafanikio.

“Wasanii ni kioo cha jamii, hebu waseme wanapata faida gani wanapofanya hivyo zaidi ya kuhisiwa tofauti na jamii? Mbona wanaweza kuwa wasanii wazuri bila ya kujichubua na kuweka dawa nywele zao?” alihoji.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...