Tuesday, January 8, 2013

HUYU NDO MTOTO ALIYEIMBA CHORUS YA WIMBO WA MSANII ROMA "2030"



Ifuatayo ni Interview kati ya HZB na Story na Baba yake.


HZB; Una miaka mingapi?
Story; sita na nusu.

HZB:Unasoma darasa langap?

Story: nimemaliza chekechea YWCA Buguruni malapa.

HZB: Baba kwa nn umeamua kumuita mwanao story?

Baba: Jina hili linanihusu mimi pamoja na yeye kwa sababu wakati anazaliwa mimi nilikua naishi hostel alipokua nikamchukua tukaishi naye, pia mimi nilikua mtoto wa mtaa,kingine yeye mwenyewe anapenda sana story hata ukiwa unamuadithia kitu anatulia kabisa, so kutokana na matukio hayo nikaona jina la story linamfaa.

HZB: Umekigundua vip kipaji cha mwanao?


Baba: Tangu alipo kuwa na miaka mitatu, mimi kazi zangu ni kuuza CD pale ilala sasa mara nyingi nikiwa na weka music naona dogo anakua anapenda zile melod na anakua anaimba mwenyewe,ila kilichonipa moyo zaidi walipewa nafasi ya kuimba shuleni kwao alifanya vizuri kuliko watoto wenzake pia alipata nafasi ya kuimba siku ya mtoto wa Africa na akafanya vizuri sana.
HZB: Ni wimbo gani alikua akipenda zaid kuimba?

Baba: Ni ule wimbo wa joti mbona usomeki,pamoja na nyimbo za willow Smith.

HZB:Nani msimamizi wa kazi zake?

Baba: Mimi mwenyewe ndo namsimamia.

HZB:Kwa umri wa Story bado mdogo sana na anaitaji kusoma sana, je atawezaje kumudu shule na muziki?

Baba:Kila kitu kinaitaji usimamizi sio kwamba muda wote atakua ana soma tu kuna muda waziada ambao tutautumia kufanya muziki, pia darasani anafanya vizuri.alishika nafasi ya nne katika watoto 42,

HZB:Amemaliza chekechea je mpango uliopo kwa sasa ni upi?

Baba: kwa sasa natafuta shule na tayar kafanya mitihani semu mbili Olimpio na Diamond

HZB:Oky nawatakia kila jema katika kazi zenu, ila nakusisitiza sana umkazie kuhusu elimu.

Baba:asante sana,atasoma tu wala usiwe na shaka.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...