Thursday, November 8, 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI DHIDI YA RUFAA YA LEMA



Wapenzi wa Chadema wakimlaki Mhe. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama leo. 
 
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa.
Mawakili wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.
Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.

Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi.

Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.


Katibu wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama Kuu leo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...