Thursday, November 1, 2012

DEREVA BODABODA AUAWA KINYAMA MKOANI IRINGA


Polisi wakiwa eneo la tukio ulipokutwa mwili wa dereva bodaboda, Abeli Nyunza.

WATU wanaodaiwa kuwa ni vibaka wamemuua kwa kumpiga na kitu kizito katika paji la uso, dereva bodaboda, Abeli Nyunza eneo la National mjini Iringa na kumpora pikipiki yake.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Muungano Frelimo mjini Iringa jirani na shule ya msingi Muungano.

Wakielezea juu ya tukio hilo, mashuhuda  wamedai kuwa majira ya usiku walisikia mlio wa pikipiki na ghafla ulizimika na baada ya hapo ilisikika sauti ikiita kwa nguvu Peter! Peter ! mfano wa mtu aliyekuwa akiomba msaada na baada ya dakika kama 10 hivi ukimya ulitanda na ghafla ulisikika mlio wa pikipiki iliyokuwa ikiondoka kwa kasi.
Mwenyekiti wa bodaboda mjini Iringa, Macurius Chengulla mbali ya kuthibitisha kifo cha dereva bodaboda mwenzao huyo bado amesema kuwa wameweka mkakati wa kuendesha msako ili kuwabana wahusika wa mauaji hayo.
Chengulla amesema kuwa matukio hayo ya kuuawa kwa madereva bodaboda kwa manispaa ya Iringa ni tukio la kwanza kwa mwaka huu japo matukio ya kutekwa na kujeruhiwa yamekuwa yakitokea .

Askari na wananchi wakitazama…

Polisi wakiwa eneo la tukio ulipokutwa mwili wa dereva bodaboda, Abeli Nyunza.

Askari na wananchi wakitazama kofia ya dereva huyo iliyokuwa imetundikwa juu ya miti.
Mwili wa dereva bodaboda, Abeli Nyunza ukiwa umetupwa katika korongo.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...