Msanii Diamond akilishambulia jukwaa la Fiesta usiku huu.
Wasanii
mbalimbali wa Bongo wakiongozwa na Diamond Platinumz, Mwana FA,
Stamina, Linah, Fid Q, Joh Makini, Shetta, Ommy Dimpoz, Nay wa Mitego,
Mwasiti na wengineo usiku huu wamefanya vilivyo katika shoo ya Serengeti
Fiesta 2012 ambapo msanii kutoka nje alikuwa Rick Ross. Wasanii hao
wametoa burudani ya aina yake kiasi cha mashabiki kushindwa kuondoka
eneo hilo mpaka kunakucha.
Wasanii wa kundi la Wanaume Family wakifanya vitu vyao stejini. Shetta akiwarusha mashabiki ndani ya Leaders Club usiku huu. Msanii Ommy Dimpoz na kundi lake wakionyesha machejo yao stejini. Linah nae akifanya vitu vyake jukwaani. Godzilla akiwapagawisha mashabiki wa Fiesta usiku huu. Shilole akiwapa raha mashabiki. wana FA kazini. Mwasiti nae akiupamba usiku wa Fiesta 2012. AT akitoa burudani kwa mashabiki waliofurika Leaders Club. Joh Makini akigani stejini. Linex akikonga nyoyo za wapenzi wa burudani. Nay wa Mitego akionyesha ukaali wa kushika mike. Amin akiwarusha mashabiki wake. Bi. Cheka akikamua sambamba na Mhe. Temba jukwaani.
No comments:
Post a Comment