Thursday, September 13, 2012

TAMASHA LA TANZANIA LIVE MUSIC KUFANYIKA SEPTEMBA 28-29 , 2012 LEADERS CLUB



Mkurugenzi wa Kampuni ya Edge Entarteinment Co Limited, Bw. Edwin akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye mgahawa wa City Sports Lounge Posta jijini Dar es Salaam wanaofuatia katika picha ni mwigizaji Jacqueline Wolper, Mwanamuziki wa zamani Juma Ubao, Hartman Mbilinyi na kutoka kushoto ni wanamuziki Mafumu Bilal na John Kitime.
Edge Entertainment Co Ltd imeandaa tamasha kubwa la muziki wa dansi linalojulikana kwa jina la Tanzania Live Music Festival litakalofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Septemba 28 – 29 mwaka huu, katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 10.00 alasiri na kuendelea.

Tamasha hili lina lengo la kukuza muziki wa dansi nchini Tanzania, kukusanya fedha kukisaidia Chama cha Muziki wa Dansi (Chamudata) kiweze kujiendesha kwa ufanisi. Kuchangia mfuko wa sanaa ulio chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
Tamasha hili litajumuisha bendi mbalimbali za muziki wa dansi nchini na litakuwa likifanyika kila mwaka, na tunatarajia kwa miaka ijayo kukutanisha bendi mbalimbali nchini na kualika bendi au wanamuziki wakubwa kuja kushiriki toka nje ya Tanzania.
Katika kufanikisha tamasha tumemchagua Jacqueline Wolper kuwa Balozi wa tamasha hili kwa mwaka 2012.
Siku moja kabla ya tamasha 27/9/2012 kutakuwa na mafunzo ya siku moja kwa wanamuziki kuhusu hati miliki yatakayotolewa na COSOTA.
Wadhamini wetu ni :TIMES FM RADIO, GLOBAL PUBLISHERS, BUSINESS TIMES na VODACOM TANZANIA



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...