Saturday, September 8, 2012

Tabora wapagawishwa na Serengeti Fiesta 2012 .


Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo jumapili litakuwa linarindima mjini Singida katika kiota cha marahaa kiitwacho Singida Motel.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.

Anaitwa Godzilla,Msanii wa hip hop katika muziki wa kizazi kipya,akiangusha mistari iliyowasisimua mashabiki mbalimbali waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.

Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishangweka vilivyo usiku wa kuamkia leo,tamasha hilo limefanyika jana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel,mkoani humo.

Nikki wa Pili akishusha mistari yake mbele ya wakazi wa mji wa Tabota.

Sehemu ya watu walivyojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Pichani kulia ni Shaffih Dauda akiwa na wadau wake.

Wakazi wa mji wa Tabora wakiwa ndani ya uwanja wa Ally Hassan Mwinyi wakati tamasha la Serengeti Fiesta lilipokuwa linaendelea.


Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua mashine,na kulia kwake ni Hamza Balla,

Moja wa zao la Serengeti Fiesta 2012,Supa Nyota Ney Lee akitumbuiza jukwaani.
Pichani juu ni msanii Recho kutoka THT akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani akisindikizwa densa wake,na chini ni mkali wa miondoko ya R&B Ben Paul akionesha uwezo wake wa kucheza na sauti mbele ya mashabiki wake.


Msanii wa muziki na pia ni muigizaji wa filamu,anaitwa Shilole akitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012,usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,mjini Tabora.

Rich Mavoko akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku

Mbunge wa Tabora Mjini,Mh Adeni Rage akisoma namba za washindi waliobahatika kujiyakulia piki pikii,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya utafiti ya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.

NI full mzuka mwanzo mwisho kwa mashabiki.

Sir Juma Nature akikamua usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 202

Watu walikuwa kibao.

Hamza Balla na marafiki zake wakiwa wamepozi ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...