Saturday, September 15, 2012

MISS KINONDONI 2012/013 HUYU HAPA...

Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni 2012/013, Brigiter Alfred akiwapungia mkono mashabiki wake muda mfupi baada ya kuvishwa taji hilo usiku wa kuamkia leojijini Dar es Salaam.
Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigiter Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana Hussein na mshindi wa tatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irene akishikilia taji la Miss Ubungo 2012. Pamoja na hayo Redd's Miss Kinondoni 2012 alijishindia taji la Miss Talent iliyokuwa umedhaminiwa na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar na wamempa zawadi ya kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka mzima
ndani ya Saloon yao.

Akivalishwa taji lake la Redd's Miss Kinondoni 2012.

Mkurugenzi wa Perfect Lady Classic Saloon, Ester Kiama ambao ndiyo waliokuwa wamedhamini Redd's Miss Kinondoni Talent akitangaza zawadi alizompatia mrembo aliyeshinda, ambaye ni Brigiter Alfred (mrembo wa katikati).

Top 5 ya Redd's Miss Kinondoni 2012. 

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...