Sunday, September 9, 2012

LOWASSA ASABABISHA MICHANGO YA SH. MIL 70 UJENZI WA KANISA LA MORAVIAN USHIRIKA WA MBEZI BEACH


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akionyeshwa picha ya mfano wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila kabla ya kuanza kwa Harambee ya Kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.Katika harambee hilo iliyoongozwa na Mh. Lowassa,jumla ya sh. Mil 70 zimechangishwa leo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipeana mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada ya Ibada ya Jumapili na baadae kuendeshwa kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.

Mwanadada aliandaliwa kwa kusoma risala ya kumkaribisha mgeni Rasmi katika kuendesha harambee hiyo, Bi. Leah Mwainyekule akisoma lisala hilo.

Bi. Leah Mwainyekule akikabidhi risala hiyo kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mkono na Mkuu wa Mstaafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Robert Mboma baada ya kuchangia katika Harambee ya Ujenzi wa kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam,uliofanyika leo, jumla ya sh. Mil 70 zimechangishwa katika Harambee hiyo.

Meneja wa Kilaji cha Kilimanjaro kutoka TBL, George Kavishe akipena mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada kuchangia katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipena mkono na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, Mzee Mwaikambo mara baada ya kuchangia katika harambee hiyo.


Kina Mama pia walikuwa Mstari wa Mbele kuhakikisha ujenzi wa Nyumba hiyo ya Mungu unafanyika kwa nguvu zote.

Balozi David Kapya pia alikuwa ni miongoni mwa waendeshaji na wahamasishaji wakubwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa hilo.

Mh. Lowassa akitoa mchango wake katika Harambee hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipokea Zawadi maalum kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada ya kuongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach,Jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyikiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach,George Nzunda akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa kwa kuendesha harambee ya Ujenzi wa Kanisa hilo iliyofanyika leo kanisani hapo.Katika harambee hiyo,Jumla ya shi. Mil. 70 zimepatikana ili kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila akitoa neno baada ya kumalizika kwa harambee hiyo.

Ibada ikiendelea kabla ya kuanza kwa harambee.

Wakuu wakiangaliwa Kwanya ya Vijana.

Mh. Lowassa akifuatilia kwanya ya vijana wa kanisa hilo.

Kwaya ikiendelea.

Waumini wakiwa katika Ibada hiyo.

Mh. Lowassa akiaga wakati wa kuondoka.


Mh. Lowassa akiagana na Balozi David Kapya mara baada ya kumalizika kwa Shunguli ya Harambee ya Kuchangia ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach,Jijini Dar es Salaam leo.
Hili ndilo Kanisa linalotakiwa kumalizika ujenzi wake ambalo harambee yake imefanyika leo na kuongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edwa

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...