Thursday, September 6, 2012

KILIMANJARO YAZIPATIA TIMU ZA YANGA NA SIMBA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA LIGI KUU



Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya micheko kwa timu za Yanga na Simba za jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Ilala.Kushoto ni Afisa habari wa timu ya Yanga,Luis Sendeu na kulia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
Zikiwa zimebaki siku tisa kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara 2012/2013, Kilimanjaro Premium Lager imezikabidhi timu za Yanga na Simba vifaa kwa ajili ya michuano hiyo.

Vifaa hivyo vimetolewa ikiwa ni sehemu ya udhamini wa jumla wa dola za Kimarekani milioni 3 (takribani TSh4bilioni) za kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager kwa timu hizo kongwe na zenye ushindani mkubwa na historia yakipee hapa nchini.Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na jezi, kaptula, soksi, vyatu vya mpira, bibs, mipira na mifuko.


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo kwa Afisa habari wa Timu ya Yanga,Luis Sendeu.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo kwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu.Katikati ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba

Picha ya Pamoja:Toka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu,Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe na Afisa habari wa Timu ya Yanga,Luis Sendeu.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...