Thursday, September 27, 2012

Jumuiya ya Uingereza- Tanzania yasherekea miaka 50‏


Balozi Dr Kamala akiwa na Sir Andy Chande

Siku ya jumanne tarehe 25.9.12 Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN- TANZANIA SOCIETY) iliandaa hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa kati ya Nchi ya Uingereza na Tanzania katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, London. Wageni mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi kuhudhuria hafla hii fupi ilioandaliwa hususani kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania. Mojawapo ya wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wetu Peter Kallaghe pamoja na mkewe Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa Britain- Tanzania Society William Fulton JP DL.
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikua ni Balozi wa Ubelgiji Mh Dr Diodorus Kamala aliyetoa mada maalum kuhusu mafanikio, maendeleo na changamoto katika nchi ya Tanzania na jumuiya nzima ya Afrika mashariki. Aidha Mh Dr Kamala alifafanua jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua kwa kasi kutokana na takwimu kutoka Benki ya Dunia pia aliongelea kuhusu masuala ya utalii, mioundo mbinu, hali ya amani na usalama ambazo zimepelekea wawekezaji wengi kuwekeza katika nchi ya Tanzania. Nchi ya Uingereza ndio nchi pekee inayoongoza katika uwekezaji katika nchi ya Tanzania Ikifuatiwa na India pamoja na Kenya
Pamoja na hayo Mh Dr Kamala aliwashukuru wana jumuiya wa Uingereza- Tanzania kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali ili kupambana na hali ya umaskini. Baada ya kutoa mada yake kulikuwa na kipindi kifupi cha maswali na majibu kutoka kwa wanajumuiya pamoja na wadau waliohudhuria.
Nae mwenyekiti wa Computer 4 Afrika ndg Aseri katanga alitoa risala fupi ya kumshukuru  mgeni rasmi kwa kujitolea kwake kuja kujumuika na wanajumuiya pamoja na hotuba yake nzuri kuhusu Tanzania.
Vile vile halfa hii ilijumuisha uoneshwaji wa picha zilizochorwa na wachoraji kutoka Tanzania ambazo zilinadiwa ili kuchangisha pesa za kuwasaidia kuwainua wadau wa tasnia ya uchoraji Tanzania. Baadhi ya wachoraji ambazo picha zao zilionyeshwa ni Mmadi Ausiy, Haji Chilonga, Hassan Kadudu, Florian Ludovick Kaija, James Haule na Aggrey Mwasha.



Balozi wa Tanzania Mh Peter kallaghe akiwa na Susan Mzee na Sheilamina
Mama Balozi Joyce Kallaghe katika picha ya Pamoja Nelly Sheilamina na Elly baada ya mkutano
Mh Balozi Dr Diodorus Kamala (Kulia) Frank Eyembe na Aseri Katanga
Mh Balozi Dr Diodorus Kamala akifanunua kuhusu maendeleo katika nchi ya Tanzania
Mh Balozi Dr Kamala akitoa mada
Mkutano Ukiendelea
Mojawapo ya picha zilizokua zikinadiwa kutoka kwa mchoraji wa kitanzania Aggrey Mwasha

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...