Saturday, September 8, 2012

Clouds yato msaada kituo cha watoto yatima Tabora‏



Sehemu ya nje ya kituo cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza kama kionekanavyo kwe mbele jioni ya leo,kituo hicho kipo nje kidogo ya mji wa Tabora,chenye jumla ya watoto wapatao 30 wanaolelewa na kituo hicho.
Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mh.Aden Rage sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya wakiwa katika picha ya pamoja na uwakilishi wa kampuni ya Clouds Media Group sambamba na baadhi ya Wasanii wa muziki wa Bongofleva ambao usiku huu wanatumbuiza ndani ya uwanja wa mpira wa Ally Hassan Mwinyi,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali wa vyakukula walioutoa kwenye kituo hicho cha ST.Francis

Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya sehemu ya msaada wa vyakula uliotolewa na kampuni hiyo kwa kituo cha ST.Francis kilichopo maeneo ya Ipuli nje kidogo ya mji wa Tabora mjini,anaeshuhudia kulia ni Mlezi wa kituo hicho Father Anthony Rajesta pia akipokea msaada huo kwa niaba kutoka kwa mkuu wa Wilaya,Shoto nyuma ya Mkuu wa Wilaya ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage ambaye pia alijitolea mipira ya mitano kwa ajili ya michezo ya kituo hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya akizungumza machache ikiwemo na kuishukuru kampuni ya Clouds Media Group na wasanii waliojumuika kwa pamoja katika tukio hilo jioni ya leo,katika suala zima la kujitolea kuisadia sehemu ya jamii kwa namna moja ama nyingine.
Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage nae akitoa shukurani zake za ujumla kwa Clouds Media Group na Wasanii wenyewe kwa kuwa na moyo wa upendo na kujitolea katika mambo mbalimbali ya kuisaidia jamii isiyojiweza kwa namna moja ama nyingine.

OfisaMahusiano wa Clouds Media Group akizunguma machache ikiwemo na kufanya utambulisho mfupi kwa baadhi ya viongo husika na wasanii wenyewe kwa ujumla.

Msanii mkongwe katika kafika anga ya muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na pia ni muigizaji wa filamu,Shilole akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.

Juunibaadhi ya wasanii waliojitokeza kushiriki katika suala zima la kuisaidia jamii isiyojiweza kwa namna moja ama nyingine.


Pichani juu ya chini ni sehemuya watoto wanaolelewa na kituo hicho wakiwa na baadhi ya walezi wao.Picha na michuzijr.blogspot.com


Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya wakiwasili kwenye kituo cha watoto yatima,St Francis kilichopo maeneo ya Ipuli,nje kidogo ya Tabora mjini.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...