Wednesday, August 22, 2012

Vurugu zaigubika Kariakoo, mabomu yalipuliwa, Chanzo mgogoro wa nyumba,mitaa yafungwa kwa muda


Mmoja wa majeruhi wa mabomu ya machozi kwenye vurugu hizo akiondolewa eneo la soko la Kariakoo baada ya kuunguka chini kutokana na milipuko hiyo, ambayo iliambatana na mawe yalikuwa yakirushwa na vijana waliokua wakitetea upande mmoja wa ugomvi huo.
Askari wa Kikosi Cha kutuliza Ghasia FFU wakiweka chini ya ulinzi mkali eneo la Kariakoo baada ya kufunga mitaa ya Kongo nay a jirani kutokana na kuibuka vurugu zilizotokana na ugonvi wa nyumba ambayo kwa maelezo ya watu wa karibu nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka 20 kati ya wamiliki na wapangaji kutokana na kutengeneza hati feki.
Mitaa ya Kituo cha Polisi Msimbazi Kriakoo ikiwa mitupu bila ya watu wengi kama ilivyozoeleka ni askari tu ndio waliokuwa wakiranda kwenye eneo hilo.
Mtu ambaye alijitambulisha kwenye nyumba hiyo ambayo inamilikiwa na mamayake, ambapo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameipigania hakiyao kwa miaka ishirini hadi leo wanaipata kutokana na kesi waliyofungua mahakamani wakidai kunyang'anywa nyumba yao na wapangaji kwa kutengeneza hati feki.a jina la Samir Sadick, alidai yeye ndie msimamizi wa nyumba hiyo
Nyumba inayo gombaniwa na kuzua tafrani kabla haijaanza kuvunjwa eneo la mtaa wa Kongo Kariakoo.


Hapa vijana wa kazi wa kampuni ya Yono Auction Mart iliyopewa tenda ya kusimamia ubomoaji wa nyumba hiyo chini ya ulinzi mkali wa pilisi wakiendelea na kazi kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Kongo
Mashuhuda nao walikuwepo tangu zoezi linaanza na walikuwepo pia wanaoufahamu mgogoro huo na kudai kuwa nyumba hiyo anadhulumiwa mzaramo na Mwarabu kwasababu anapesa, lakini wengine wakasema nyumba hiyo imeuzwa mara tatu tofauti na kuzua mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...