Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo ambapo amewataka vijana kujitambua na kuwa na mikakati endelevu na kukaa kama vikundi ili Serikali iweze kuwasaidia kupata misaada na kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 11 Agosti na kutimiza malengo aliyokuwa akiyatafakari baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere juu ya Vijana.
Umati wa wakazi wa Temeke katika tamasha la siku ya maadhimisho ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambako zilifanyika shughuli mbambali ikiwemo Ujumbe kutoka Serikalini na Kupima virusi vya Ukimwi bure.
Baadhi ya Vijana wakitazama machapisho ya vijarida mbalimbali vinavyotoa taarifa kuhusiana na Afya zao na jinsi ya kupata huduma.
Mpiga picha Jofrey Mwakibete akipima Presha katika hatua za kuelekea kupima maambukizi ya VVU ikiwa ni kuhamasisha Vijana wenzake kujitambua kama wameathirika.
Mmoja wa wakazi wa jijini Dar es Salaam akicheki Afya yake.
Wakazi waliohamasika kupima VVU na magonjwa ya Zinaa wakiwa katika foleni ya kupata huduma hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya vijana Duniani katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar.
Mpiga picha Jofrey Mwakibete akipima Virusi vya Ukimwi.
Meza Kuu ikongozwa na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akikagua Timu ya soka ya Vijana ya Wanawake ya Evergreen kkutoka Temeke ambayo ilipambana na Timu ya Mburahati Queens kuonyesha ushirikiano wa Vijana akiwa ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Maria Khan na Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Dkt. Festus Ilako.
Mheshimiwa mgeni rasmi hapa akikagua timu ya Mburahati Queens.
Pichani Juu na Chini Kipute kati ya Mburahati Queens na Evergreen Queens ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Evergreen kushinda 2-1.
HABARI/PICHA: JANE JOHN BLOG
No comments:
Post a Comment