Friday, August 3, 2012

TIGO YAZINDUA PROGRAMU YA MAJARIBIO YA 'TIGO KILIMO'



Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tigo yazindua suluhu kwa wakulima kupitia mtandao wa simu za mikononi

Agosti 1, 2012, Dodoma. Tigo leo imetangaza uzinduzi wa programu ya majaribio inayojulikana kama ‘Tigo Kilimo’ ambayo inakusudia kuwapatia wakulima taarifa stahiki kwa wakati muafaka za kilimo kupitia simu zao za mikononi.

Tigo Kilimo inatumia teknolojia ya ujumbe wa maadishi ( sms) ambayo itawapatia wakulima wadogo wadogo fursa ya kipekee kuboresha shughuli zao. Kupitia Tigo Kilimo wakulima watapata taarifa za hapo kwa hapo kuhusu hali ya hewa na taarifa nyinginezo za kilimo. Hii itawasaidia kuongeza mavuno na kupunuguza utofauti ya mavuno na sehemu nyingine za ulimwengu.

“Kwa kutumia mtando wa simu za mikononi kuleta suluhu kwenye maswala ya Kilimo wakulima wataunganishwa kwa ukaribu zaidi na italeta ufanisi zaidi katika shughuli za kilimo ,” alisema Yaha Ndojore , Meneja Mradi wa huduma za Tigo Kilimo , Tigo Tanzania . “Kutokana na miundombinu na mawailiano hafifu kwenye sehemu kubwa za nchi zinazoendelea , wakulima wanataabika kupata taarifa muhimu za kilimo , pamoja na mafunzo na ushauri kuhusu maswala kama wadudu na magonjwa , hali ya hewa na mbinu tofauti za kilimo . Kupitia huduma hii , Tigo itatoa fursa ya suluhu mpya na nafuu yakusaidia hizi changamoto.” Alisema

Kama mdhamini mkuu wa mawasiliano ya maonyesho ya Nane Nane na kusheherekea Wiki ya Maonyesho ya Kilimo,Tigo inawapatia wakulima mawasiliano ya Tigo Kilimo bure kwa mwezi mzima wa Ogasti.Wakulima wanaweza kupata huduma hii kupitia simu zao za mikononi kwa kupiga *148*14# na kupata listi ya huduma za Tigo Kilimo. Hapa watapata lisiti ya taarifa mbali mbali kwa ujumla kuhusu hali ya hewa , udani wa menjimenti wa udongo , njia ya kudhibiti wadudu kwa zaidi ya aina 20 za mboga , matunda na nafaka , taarifa kuhusu utunzaji wa mifugo nk. Kwenye awamu ya pili ya huu mradi Tigo itaongeza huduma kama vile bei ya bidhaa sokoni, na kuanzisha huduma kwa wateja wakulima, ambao wataweza kupiga wakiwa na maswali mbali mbali

Simu za mikononi zinarahisisha mawasilano. Tigo inaweza kuwafikia wakulima viijini na taarifa muhimu kupita huduma hii. Kwa kupitia Tigo Kilimo , wakulima wanapata ujuzi wa kuboresha kazi na stadi zao ambazo zitasaida kuongeza mazao , kupunguza gharama na kuongeza kipato, na wakati huo huo kupata faidia kwa kutumia simu za mikononi.


KuhusuTigo

Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 tanzania Bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshwaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano mpaka katika kutoa huduma za intanet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia Tigo Pesa.

Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...