Monday, August 27, 2012

TBL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA "MALTIZA" KISICHO NA KILEVI KINACHOTENGENEZWA NA KIMEA HALISI CHA HAPA NCHINI TANZANIA


Kundi la SKYLIGHT Band likishambulia Jukwaa kabla ya uzinduzi wa Kinywaji Kipya kinachozalishwa na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) cha MALTIZA kinachotengenezwa na Kimea halisi kisicho na kilevi uliofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar leo.
Malkia wa SKYLIGHT Band inayokuja kwa kasi jijini Aneth Kushaba (mbele kulia) sambamba na Mariam Lucas wakikonga nyoyo za Wakazi wa Dar waliohudhuria uzinduzi huo.
Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam (katikati) akikaribisha wageni kuhudhuria uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika leo jijini Dar.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiorodhesha majina yao kwa warembo maalum waliondaliwa kupokea wageni na kushiriki bahati nasibu ya papo kwa hapo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha MALTIZA.
Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kuzinduliwa kwa kinywaji hicho kipya kinachopatikana katika ladha mbili za APPLE na PINE (Pineapple) ambacho amefafanua kwamba Tanzania imekuwa ya kwanza kwa Afrika kuzindua kinywaji cha aina hiyo kisicho na kilevi chenye ubora na kinachotengenezwa na kimea halisi kinachozalishwa hapa nchini.
Bi. Consolata Adam amesema kinywaji hicho kinapatikana katika ujazo wa 330Mls na kimeshasambazwa nchini kote na bei yake ni shilingi 1500, aliongeza kuwa kinywaji hicho ni halisi kisichotiwa rangi na kuwataka Watanzania kujiburudisha na MALTIZA.
Bi. Consolata Adam akionyesha kopo za Ujazo wa 330Mls za kinywaji cha MALTIZA aina ya APPLE na PINE.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...