Saturday, August 25, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LAZINDULIWA KWA KISHINDO MJINI MOSHI


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Leonidas Gama akimtaja mshindi aliyejinyakulia gari aina ya Vits iliyokuwa ikinadiwa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,maara baada ya kuchezeshwa droo usiku wa kuamkia leo,pichani mwanzo kulia ni Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru,Muwakilishi kutoka michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Abdallah Mohamed akishuhudia tukio hilo,na mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini,Mh Dr Msengi wakishuhudia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh Leonidas Gama sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini, Mh Dr Msengia wakiingia kwa shangwe kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kulizindua tamasha hilo ambalo limepokelewa vyema kwa wakazi wa mji huo na vitongoji vyake. Pichani kulia ni Dj Zero akikamua vilivyo.

Dj Pq kutoka Clouds FM akikamua vilivyo kwenye mashine,kati ni mtangazaji wa Clouds FM B Dozen na mdau mwingine wakifuatilia kwa makini makamuzi yanayoendelea usiku wa kuamkia leo,ambapo washabiki kibao walijitokeza ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika.



Pichani shoto ni msanii kutoka THT,Recho sambamba na wacheza shoo wake wakitumbuiza jukwaani usikuwa kuamkia leondani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Moja ya kikundi mahiri kutoka THT kkikionesha mbwembwe zake jukwaani.



Dj Zero akikamua vilivyo.

Moja ya kikundi cha THT kikiwa katika picha ya pamoja.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa chuo cha Ushirika mjini Moshi.





Baadhi ya wasanii nyota wa filamu nchini nao wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta.

Hapakutosha usiku wa jana.


Msanii wa kizazi kipya Sheta akiwaimbisha washabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku wa kuamkia leo ndani ya tamasha la Serengeti.







Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza usiku wa kuamkia leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012

Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi.

Mmoja wa wasanii wa hip hop Joh Makini akikamua vilivyo usiku wa kuamkia leo mbele ya umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tamasha la Fiesta.

Msanii mahiri wa bongofleva,Lina akiwa na densaz wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.

Lina akiimba wimbo wake Yalaiti

Mkali mwingine wa hip hop Mwana FA akishusha mitindo huru.

Pichani juu na chini Mwana FA akilishambulia jukwaa vilivyo kwa mitindo yake huru iliyokuna vilivyo mashabiki wake,waliofika kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.


Wasanii wa nyota wa Filamu hapa nchini nao walijumuika kwa pamoja kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani jukwaani ni Wema Sepetu,Jacob Steven a.k.a JB,pamoja na Aunt Ezekiel wakilisakata sebene.

Ray nae akilisakata sebene vilivyo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...